Kamikaze agonga msumari wa mwisho kwa Vanessa Mdee

Jumatano , 11th Dec , 2019

Rapa anayewakilisha pande za Singida, Cyrill Kamikaze, amegongelea msumari wa mwisho kwa Vanessa Mdee na kusema, alivyomtolea lugha chafu hadhani kama alimaanisha ila alikuwa na hasira na mawazo na kwamba hawezi kumjibu chochote.

Msanii wa muziki Bongo, Cyrill Kamikaze na Vanessa Mdee.

Kamikaze ameeleza hayo mbele ya kamera za EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuwa  alichukuliaje kauli ya Vanessa Mdee, kumwambia hapendi wanaume ambao wana tabia za kike ambapo amejibu.

"Hilo lishapita labda tuweke msumari wa mwisho, sikuwahi kufanya chochote wala kuongea lolote kitu kilichotokea ni kati yake na Jux kwenye mapenzi yao, mimi sijawahi kuingilia na kujua chochote kama aliongea hivyo ni fresh"  amesema Cyrill Kamikaze.

Aidha Kamikaze ameongeza kuwa "Kwa yeye kuongea vile sijui alikuwa katika hali gani na alimaanisha nini, sijawahi kukaa naye kumuuliza lakini nina imani hakuongea kile kitu kwa kukimaanisha, unajua kuna muda unaweza ukaongea kitu kwa kuwa una hasira au mawazo kwa sababu ya vitu vingi, sijawahi kumhukumu na siwezi kurudisha neno lolote".