Kampeni ya Mama la mama kuzinduliwa leo

Jumamosi , 1st Mei , 2021

Kuelekea siku ya mama duniani Kampuni ya East Africa TV inazindua rasmi Kampeni ya Mama la mama ambayo ni inahusu kusheherekea kazi kubwa wanazozifanya wakina mama kwenye familia zao.

Picha ya baadhi ya wafanyakazi wa kike kutoka East Africa TV wakiwakilisha Mama la mama

Kampeni hiyo itazinduliwa leo Mei Mosi Samaki Samaki Mlimani City na itakuwa inashirikisha wananchi mbalimbali kueleza kwanini anahisi mama yake anastahili kuwa mama la mama ambapo mshindi atapata zawadi za thamani.

Baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa kampeni hiyo ni Tsh Milioni 1 ambayo itaingizwa kwenye Akaunti ya UBA na jiko la kupikia la kisasa lenye thamani ya Tsh Laki 7 kutoka Jaden Home Store.

Zawadi zingine ni king'amuzi cha  DSTV na malipo ya kifurushi cha juu cha Premium , bidhaa za urembo kutoka Atsoko zenye thamani ya Milioni, Sabuni za OMO, pamoja na chakula cha mchana na watoto wake kwenye hoteli ya Levant iliyopo Masaki Dar es Salaam.