Jumamosi , 3rd Jan , 2015

Katika wakati huu ambao mitaa inasubiri kwa hamu Video ya muziki ya "Kiboko Yangu" kutoka kwa rapa Mwana FA, star huyu wa muziki amewahakikishia mashabiki wake ujio wa video bora kabisa kuliko zote alizowahi kufanya.

Ali Kiba na Mwana FA

amesema imani hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa alioufanya katika kazi hiyo.

MwanaFA ambaye amekiri mwenyewe kutokuwa na rekodi ya kufanya video kali, akijitetea kuwa hii pia inatokana na aina ya muziki anaoufanya, amesema kuwa kwa sasa licha ya changamoto ya muda na shughuli nyingi,cut ya kwanza ya Kiboko Yangu inatarajiwa kumfikia ndani ya siku hizi mbili.