Jumatatu , 28th Aug , 2017

Msanii wa bongo fleva na mkali wa R&B, Rama Dee amefunguka kwa kuwataka vijana kuchangamkia fursa ya ajira inayotokana na mchezo wa mpira wa kikapu ili waweze kuondokana na janga la utegemezi katika familia pamoja na kujiinua kiuchumi.

Msanii wa bongo fleva na mkali wa R&B, Rama Dee.

Rama Dee amebainisha hayo muda mchache alipowasili katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay JIjini Dar es Salaam, ilipokuwa ikifanyikia fainali za Sprite BBall Kings 'game 4' baina ya TMT dhidi ya Mchenga BBall Stars na kuwaomba wazee wawe tayari katika kuekeza katika michezo hasa mpira wa kikapu ili uweze kusonga mbele zaidi kama walivyoamua kufanya uongozi wa EATV pamoja na Sprite.

"Binafsi nawashukuru EATV LTD kwa kushirikiana na Sprite kuweza kuupa kipaumbele mchezo wa basketball kwa kuwa ulikuwa unapotea kabisa. Vijana sasa wanapaswa waamke na kuchangamkia fursa iliyopo katika mpira wa kikapu kwa kuwa inatoa ajira",alisema Rama Dee. 

Mtazame hapa chini anavyofunguka mengine zaidi.