Jumanne , 19th Aug , 2014

Tamasha kubwa la burudani ya muziki, Kilimanjaro Music Tour 2014 sasa linaelekea huko mjini Kigoma ambapo Jumamosi hii tarehe 23, moto wa Burudani usiyo na kipimo utawashwa na mastaa wakali live stejini katika uwanja wa Lake Tanganyika.

msanii wa muziki Mwana Fa akitumbuiza Kili Music Tour 2014

Wasanii watakaotokisa jukwaa ni pamoja na Amini, Proffesa Jay, Ben Pol, Mzee Yusuph, Mwana Fa, Christian Bella, Weusi, Mwasiti na Diamond Platnumz.

Timu nzima ya East Africa Radio na East Africa TV akiwepo Mjukuu wa Ambua, Zembwela Mfalme wa Amani na DJ Mafuvu watakiamsha mbaya.

Milango itafunguliwa saa 10 jioni na kiingilio kitakuwa ni shilingi 3,000 tu mlangoni, bia moja bure, kutakuwa na Chakula na vinywaji mbalimbali.

Kili Music Tour 2014, Tunazungusha kikwetu kwetu.