Jumamosi , 12th Dec , 2020

Msanii wa Singeli Balaa Mc amesema aliogopa kushea video clip ambayo ili-trend mitandaoni kipindi cha uchaguzi ikionyesha kikosi cha kutuliza ghasia 'Field Force Unit' wakiwa wanaimba wimbo wake wa 'nakuja'.

Msanii wa singeli Balaa Mc

Akifunguka kupitia EATV & EA Radio Digital, kuhusiana na hilo Balaa Mc amesema aliogopa kupost  kwa alihofia kufuatwa nyumbani na kikosi hicho ila baadaye akagundua kuwa ilikuwa ni sapoti na watu kukubali anachokifanya.

"Nilivyoona ile clip niliogopa kwanza niliwambia hadi meneja wangu, niliogopa kwamba nisije nikapost halafu wakanifuata nyumbani ila nimegundua wao wamekubali kitu ambacho nimekifanya, kuna mmoja kati ya wale kwenye kile kikosi alinicheki, nikakutana naye na tukaongea ninawashukuru sana" amesema Balaa Mc 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.