Jumamosi , 20th Jul , 2019

Mwimbaji Christian Bella, amewajibu wale wote ambao wanamsema Hamisa Mobetto kwamba hajui kuimba, pia amemchana msanii na mfalme wa Bongo Fleva Ali Kiba.

Christian Bella, Hamisa Mobetto na Alikiba

Christian Bella amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital na kusema wapo mastaa wengi hawajui kuimba na wamuache Hamisa Mobetto.

"Tukitaka kuchambua watu wasiojua kuimba ni wapo wengi, kuna watu wengi ni mastaa lakini sio wakali wa kuimba wanatengenezwa studio, tusimjaji tu Hamisa, siwezi nikamtaja mtu kwamba hajui kuimba ila tukitaka kwenda kwenye vigezo tutafika huko, wanapiga "verse" kila baada ya sekunde tano wanaonganisha na ni mastaa tu".

Pia amesema kinachondelea kati yake na Hamisa Mobetto ni kazi tu hakuna mapenzi kama watu wengi wanavyodhani na wanampango wa kuandaa tamasha kubwa la kimuziki hapa nchini Tanzania.

Aidha msanii huyo amemchana Mfalme na Staa wa Bongo Fleva Ali Kiba, kwa kumwambia huwa anamuudhi sana tabia yake ya kupenda zaidi mpira kuliko muziki, na alishamwambia aachane na mpira ili wafanye muziki lakini Ali Kiba haelewi.