Alhamisi , 16th Jan , 2020

Msanii wa muziki Shilole, amewataka mashabiki zake wasimpande kichwani kwa kumuuliza kwanini hapati mtoto na mumewe kwa sababu hawajui ana matatizo gani.

Picha ya Shilole na mumewe Uchebe

Akifunguka kupitia EATV & EA Radio Digital, Shilole amewataka mashabiki zake wawe wavumilivu na wasijaji maisha yake, bali wafuatilie kazi na biashara zake.

"Tutapata mtoto tu, halafu hayo sio mafungu ya nyanya kwamba yanawekwa tu pale, ni baraka kutoka kwa Mungu, bado siku haijafika hata mimi natamani sana kupata mtoto, naamini ataleta kheri kuhusu mashabiki zangu siwajali kwa sababu wao hawalali na mimi" amesema Shilole.

Pia Shilole ameendelea kusema "Wao wanajua kama nina matatizo gani au walishanipeleka hospitali wakajua kama nina shida gani, kwahiyo wawe wavumilivu wasijaji maisha yangu, waangalie muziki wangu na biashara zangu mambo ya ndoa yangu na kutozaa hayawahusu nikipata waseme Inshaalah, nikikosa waseme Hewala" ameongeza.