Kwa mujibu wa taarifa hiyo, marehemu Spack anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho nyumbani kwao mkoani Tanga, ambapo mazishi yataanza majira ya saa nne asubuhi.
Taarifa hii imepokelewa kwa huzuni na mashabiki pamoja na wadau wa burudani, wakionyesha salamu za rambirambi na kumuombea marehemu apumzike kwa amani.




