
Khaby Lame
Khaby alizaliwa Machi 9, 2000 nchini Senegal, baada ya mwaka mmoja wazazi wake walihamia nchini Italia na ndipo anapoishi mpaka sasa.
Miaka miwili iliyopita Khaby aliachishwa kazi katika kiwanda alichokuwa anafanya kazi katika mji wa Turin, Italia. Baada ya hapo akiwa nyumbani alianza kutengeneza madhui na kuweka katika mitandao ya kijamii. Na mwaka huo nchi nyingi barani Ulaya zilkuwa kwenye karantini.
Video za Khaby zilisambaa na kupata umaarufu kutokana namna ambavyo alikuwa akiigiza kazi zilizofanywa na watu kwa kutumia nguvu nyingi, yeye alizifanya kwa urahisi bila kusema chochote katika video.
Ubunifu huo ulimpa mashabiki wengi ulimwenguni, na mashabiki walianza kumtumia video za watu wanaofanya kazi rahisi kwa njia ngumu ili azifanyie maigizo.
Sura yake imetumika katika kutengeneza vibonzo vingi mtandaoni, Mei 3 mwaka huu jarida la Forbes lilimtaja katika orodha ya vijana 30 barani ulaya waliobadilisha biashara na jamii kwenye upande wa sanaa.
Khaby anakadiriwa kuingiza dolla milioni 6 sawa na Tsh bilioni 13 kwa mwaka kupitia mtandao wa TikTok na Instagram.