Ijumaa , 15th Aug , 2014

Msanii wa muziki Mwana FA amewataka mashabiki wake kuvuta subira wakati huu ambapo video yake ya ngoma ya Mfalme ipo katika hatua za
mwisho za maandalizi, kabla ya kuiachia rasmi hivi karibuni.

msanii wa muziki wa bongo Mwana Fa

Mwana FA amesema kuwa, video hii kwa sasa ipo katika mchakato wa kuboreshwa zaidi, ambapo Director wake amekuwa akitumia muda zaidi kuiongezea baadhi ya vitu, kazi ambayo itakamilika ndani ya wiki Mbili ama Tatu zinazokuja.