Ijumaa , 7th Oct , 2016

Zikiwa zimepita siku kadhaa toka watani wa jadi Simba na Yanga kukutana na kuoneshana ubavu kwa kutoka sare ya bao moja kwa moja, mwanamuziki Lady Jaydee ambaye sasa ameachia video yake mpya ya 'Sawa na Wao' amesema kuwa yeye ni shabiki damu wa Yanga

Lady Jaydee

Zikiwa zimepita siku kadhaa toka watani wa jadi Simba na Yanga kukutana na kuoneshana mabavu kwa kutoka sare ya bao moja kwa moja, mwanamuziki Lady Jaydee ambaye sasa ameachia video yake mpya ya 'Sawa na Wao' amesema kuwa yeye ni shabiki damu wa Yanga.

Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Facebook leo alipokuwa akichat na mashabiki zake amesema kuwa yeye ni shabiki wa Yanga damu kwa Tanzania na nje ya nchi timu anayoipenda ni Chelsea japo anadai kwa sasa amekuwa si mfuatiliaji sana wa soko kutokana na mambo yake kuwa mengi na majukumu ya hapa na pale.

"Mimi ni shabiki wa Yanga damu na nje naifuatilia sana Chelsea lakini saizi sifuatilii mpira sana kihivyo siku hizi" alisema Lady Jaydee

Msanii Lady Jaydee leo usiku atakuwepo live kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV ambapo atafunguka mambo mengi kuhusu muziki wake na mipango yake katika muziki wa Bongo Fleva.