Ijumaa , 8th Jan , 2016

Wasanii wa muziki Gramps Morgan kutoka kundi la Morgan Heritage wameanza kuwekeza nchini Kenya ambapo wanatengeneza studio yao ambayo itakuwa ikifanya kazi sambamba na biashara nyingine ya bidhaa za chakula zikitengenezwa chini yao.

wasanii wa muziki kutoka kundi la Morgan Heritage

Mipango yote hii miwili kwa sasa ipo katika hatua za awali ambapo biashara yao itafanyika kwa kushirikiana na wadau ambao watawekwa wazi pale taratibu za makubaliano zitakapokamilika.

Hatua hii kutoka Morgan Heritage inakuja baada ya kutangaza mapenzi yao kwa Kenya na nia ya kuhamia nchini humo ambapo wameanza kwa uwekezaji, wakiwa pia na rekodi ya kushiriki katika shughuli kadhaa za hisani nchini humo.