Jumapili , 15th Aug , 2021

Mchekeshaji JK Comedian amefunguka msala ambao amewahi kukutana nao akiiga sauti mbalimbali za viongozi wa kisiasa kwa kusema aliwahi kupokea simu za vitisho.

Picha ya JK Comedian

JK Comedian anasema kuna watu walimpigia simu kupitia sauti za viongozi wa vyama vingine kwamba anawafanyia hujuma kwa kuvuja kwa sauti za waheshimiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mpaka sasa mchekeshaji huyo anaweza kuiga sauti mbalimbali kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Joseph Mbilinyi, Afande Sele na wengineo.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.