Msanii akiri kufanyiwa maajabu na Pierre

Jumatano , 22nd Mei , 2019

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amesema watu ambao walikuwa hawamuelewi Pierre Liquid kuwa anakipaji gani, sasa wanafahamu kuwa Pierre ni msanii wa muziki pia ni mchekeshaji wa maigizo.

Beka Fleva ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika kipindi cha eNewz cha EATV ambapo amedai sasa hivi watanzania wanatakiwa wamuelewe Pierre ni mchekeshaji anayeimba muziki.

"Kwa audio ya kwanza hii ya 'Lamba Lolo' kiukweli viewers wake wamekimbia, video zangu nyingi huwa zinakimbia lakini audio huwa zinasuasua, ila nahisi kwa sababu nimechanganya nguvu ya msanii kutoka sekta nyingine ya bongo muvi upande wa komedi, Pierre Liquid", amesema Beka Flavour.

"Niliamua kumtumia Pierre kwenye ngoma yangu kwa ajili ya kutengeneza utofauti katika ngoma yangu ili watu wajiulize Pierre kaimba nini ndiyo maana watu wengi wanaenda kusikiliza Pierre", ameongeza Beka.

"Kuhusu kunigomea kutokea kwenye video yangu sio kweli, hawezi kuniletea mambo hayo ya kuzingua, ila nimechelewa kutoa video kwa sababu nimeona audio imefanya vizuri sana kwa hiyo nitatoa baada ya wiki 2 au 3".

Kwa sasa wawili hao wanatamba na wimbo wa Lamba lolo ambapo Pierre na yeye ameingiza vionjo vyake.