Msanii CPwaa afariki Dunia, familia yaeleza chanzo

Jumapili , 17th Jan , 2021

Msanii Ilunga Khalifa almaarufu CPwaa amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Januari 17, 2021, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambako alipelekwa kupata matibabu baada ya kuzidiwa ghafla.

Msanii CPwaa enzi za uhai wake

Ndugu yake wa karibu Murad Omary, ameithibitishia East Africa Radio huku akiweka wazi kuwa msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Nimonia.

'Cpwaa alilazwa Muhimbili ICU tangu Jumatano ambapo alikuwa anasumbuliwa na tatizo la Nimonia na usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba au saa nane hivi tukapigiwa simu kutoka Muhimbili kuwa amefariki'', amesema Murad Omary.

Aidha Murad Omary amesema msiba upo Magomeni kwa mama yake mzazi na CPwaa na mazishi yanafanyika leo saa 10:00 jioni kama hakutakuwa na mabadiliko ya ratiba iliyopangwa baada ya kikao cha familia.
 

Tazama video hapo chini Murad akieleza zaidi