Ijumaa , 2nd Jul , 2021

Unaweza kusema mambo yote yatapita lakini muziki utabaki milele kwani ardhi ya Tanzania ilibarikiwa wasanii ambao walitupeleka “Matawi ya Juu” kwa mtindo wao na tungo tamu ambazo hata ukikesha kama “CNN” huwezi acha “Sikiliza”.

Picha ya Wasanii Mangwair na Langa

 

Ukweli ni kwamba “Upweke ni Uvundo”, na uhalisia utabaki kuwa mashabiki wa muziki wa Hip Hop bado uvundo unawapeleka mbio mbio kwani na imani endapo ushikaji wao wa damu waliokuwa nao The Late Albert Mangwea na Langa wangekuwa walifanya japo hata wimbo mmoja wa pamoja basi hii leo huwenda mashabiki wangelikuwa wame-chill ghetto linalonukia utuli safi huku wakiendelea na Party fulani hivi wakifurahia ubunifu na sanaa yao.

Sikiliza zaidi hapa