"Nimevaa 'kauka nikuvae' mwezi mzima"- Ommy Dimpoz

Jumanne , 2nd Jul , 2019

Msanii nguli wa Bongo Fleva ambaye anatamba na wimbo wake mpya wa 'One & Only', Ommy Dimpoz amezungumzia maisha yake ambayo aliishi kipindi anatafuta nafasi ya kutoka kimuziki.

Ommy Dimpoz

Ameyasema hayo akipiga stori na eNewz ya EATV, ambapo amesema kuwa anayafahamu maisha yote ya mtaani kwa hiyo sasa ni wakati wake wa kula maisha.

"Mimi nimeishi maisha yote unayoyajua wewe, sijui zile za chumba kimoja uswahilini, vila unavaa nguo moja mwezi mmoja kauka ni kuvae ni, kwa hiyo unapopata nafasi itumie vilivyo maisha haya ni mafupi", amesema Dimpoz.

Aidha Ommy Dimpoz alionekana kutofurahishwa na kubadilika sura baada ya kuulizwa kuhusu maisha halisi ya baba yake, ikidaiwa kuwa hapeleki huduma nzuri kwa baba yake.

Mtazame hapa akijibu kuhusu hilo