P-Funk Majani na Profesa Jay
P-Funk ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital ambapo amesema, “ile 'comment' ina kitu ambacho kimejificha kuhusu Prof. Jay ambaye ameweka majungu, roho inamuuma hii 'issue' sio ya leo wala ya jana ni zaidi ya mwaka umeshapita, ile meseji inajieleza imenibidi nitoe ya moyoni maana nampigia simu hapokei ananikwepa”.
Aidha 'Producer' P-Funk Majani ameendelea kusema kuwa heshima ya Prof Jay imeshuka kwa sababu suala hilo la pesa walishalimaliza ila Prof.Jay anaendelea kuchochea na kuwa na roho mbaya, ulafi hata picha zake ha-likes kwenye mitandao ya kijamii na hawajawasiliana kwa mwaka sasa.
Pia P-Funk Majani amesema Prof. Jay ni mbinafsi anapenda afaidike yeye na hapendi wenzake wafaidike na kwamba huwa anafanya kazi kujuana, hata kulipa pesa hadi ipite mwaka tofauti na wasanii wengine.

