Alhamisi , 16th Sep , 2021

Last King Of 90’s, Rapcha amekanusha taarifa za kupangiwi cha kuzungumza awapo kwenye interviews na bosi wake P-Funk Majani baada uvumi kuenea kuwa kuna baadhi ya vitu hatolei ufafanuzi kutokana na kubanwa koo.

Picha ya Msanii Rapcha

Akipiga stori na East Africa Tv, msanii huyo wa Bongo Records amesema haijawahi tokea akazuiliwa au kupangiwa vitu vya kuzunguma kwani ana amini yeye sio miyeyusho.

"Haiwezi kutokea kitu kama hicho, ujuwe mpaka mtu anakupangia cha kuzungumza basi anajua kuwa huwa unafyatuka ila kwa mtu ambaye ana amini katika msanii wake na anajuwa kuwa hana miyeyusho hawezi kumpangia cha kuzungumza" - Rapcha