Jumatatu , 28th Dec , 2020

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza umewasili leo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere International Airport, ukitoka Jijini Dodoma na kufikishwa nyumbani kwake Kibamba, Luguruni Dar Es Salaam.

Jeneza lililobeba mwili wa Godfrey Mngereza ukiwa nyumbani kwake Kibamba

Kinachoendelea kwa sasa baada ya kufikishwa kwa mwili huo ni ibada na kuaga mwili kisha utarejeshwa katika Hospitali ya Lugalo ambapo siku ya Disemba 29 utapelekwa kuagwa tena kwenye ukumbi wa Karimjee.

Baada ya hapo mwili utasafirishwa mpaka Same Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika siku ya Jumatano Disemba 30 kuanzia 7:50 Mchana.

Godfrey Mngereza alifariki dunia usiku ya kuamkia sikukuu ya Christmas katika Hospitali ya General iliyopo Jijini Dodoma wakati akipatiwa matibabu.