'Sifanyi kimazoea' - Rich Mavoko

Jumatano , 11th Sep , 2019

Akifanya mahojiano na show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, Rich Mavoko amefunguka kuhusu mabadiliko yake kimuziki, ambayo yamekuwa yakiongelewa na mashabiki kadhaa wanaosema ameanza kupotea kimuziki kwa kile wanachodai kufanya staili ambayo haiendani naye.

Rich Mavoko

Rich anasema mabadiliko ni kawaida kisanaa ili kuongeza mashabiki na zaidi kuchangamsha akili ili usionekane ni mtu yule yule na mipango ndiyo humfanya mtu kubadilika kwa sababu huwezi kufanya jambo moja kwa staili iliyozoeleka.

"Nimefanya nyimbo nyingi za mapenzi, kuna muda inabidi ubadilike kufuata upepo unavyoenda lakini asili yako bado itabaki vile vile hivyo unaweza kubadilika lakini asili yako haipotei,” alisema.

"Ukitaka kwenda mbele kwa sasa lazima ubunifu uongezeke hivyo unapofanya vitu tofauti kwanza ubongo unakua kama hii ngoma ya 'Babilon' nimeamua kufanya kitu cha utofauti nje ya vile watu wengi walikuwa wanategemea”.

"Nilifikiria kuimba kuhusu mama lakini mimi sifanyi kitu kimazoea, kuna watu wanatutazama pia ambao inabidi tuwape somo hivyo siwezi kufanya kitu kile kile,” aliongeza.