Sitoacha kukopi- Banana Zorro

Alhamisi , 6th Dec , 2018

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Banana Zorro amefunguka kuwa hatoweza kuacha kupiga kopi kwakuwa wateja wake wengi wanapenda yeye aimbe kopi licha ya wadau kuhoji kwanini amekuwa akiimba aina hiyo ya muziki kwenye maonesho yake.

Msanii, Banana Zorro.

Akiongea kupitia eNewz Banana amesema kuwa wateja wake wengi wamekuwa wakimtaka yeye afanye kopi za baadhi ya wasanii ambazo zinakuwa tayari zilishaimbwa japo kwa upande wake haoni kwamba ni tatizo kwa kuwa yote hiyo ni sanaa.

"Mimi mara nyingi nimekuwa nikiimba kwenye kwenye Balozi ya nchi mbalimbali na mara nyingi unakuta naitwa kwenye balozi mfano nimeitwa ubalozi wa China na unakuta wanataka niimbe nyimbo za china tu, ila naendelea kuwashawishi ili waweze kuelewa miziki yetu na sasa", amesema Banana.

Banana ambaye anatamba na kibao chake cha 'Sitanii' ameongeza kuwa kila mtu ana namna ya kutafuta pesa hivyo yeye anawapigia wazungu na wajerumani hivyo anapiga nyimbo ambazo zitaweza kuendana na mashabiki zake na wale ambao anataka waenjoy kupitia band yake.