
Msanii Skales
Skales ameeleza hayo baada ya kuona habari inayoendelea kwa sasa nchini kwao Nigeria, inayohusu kesi ya kubaka na kunyanyasa kingono kwa mchungaji aitwaye Biodun Fatoyinbo.
"Mama yangu alifanyiwa kitendo cha kikatili kwa kunyanyaswa kingono na kudhalilishwa na baba yangu, mbali na vitendo vyote hivyo bado alikuwa chini ya baba, alikuwa anafanya vitu vya kipuuzi kutoka na wanawake wengine, nilikataa kwenda kukaa naye nilibaki na mama yangu na nilishuhudia hayo yote nikiwa na miaka mitano" alitweet msanii Skales.
Mastaa wengi sana wameonekana kukemea na kukasirishwa na kitendo cha mchungaji huyo, Skales yeye alitumia mtandao wa kijamii wa Twitter, kueleza kile kilichomkuta mama yake kipindi yeye alipokuwa na umri wa miaka 5.