Alhamisi , 28th Jul , 2016

Shindano la Dance100% linaingia katika usaili wake wa mwisho kwa mwaka 2016 wiki hii siku ya Jumamosi ambapo baada ya hapo makundi yaliyoshinda awamu ya kwanza na ya pili na yatakayoshinda Jumamosi yatachuana kwenye robo fainali.

Majaji wa Dance100 2016

Akizungumza na EATV mmoja wa waratibu wa shindano hilo Bi. Bhoke Egna amewataka vijana washiriki na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika usaili wa Jumamosi kwani usaili huo ni burudani tosha ya bure kwa watu wote watakaojitokeza.

''Usaili huo kwa makundi utakuwa ni wa mwisho ambapo hatua inayofuata ni makundi 15 kuanza hatua ya robo fainali, nusu fainali, na fainali yenyewe hivyo usaili wa Jumamosi hiii pia unalenga kupata akundi matano'' Amesema Bi. Bhoke

Ameongeza kuwa kama kawaida hakuna kiiingilio katika ushiriki wa shindano hilo na vijana ambao wana umri wa miaka 18 na kuendelea wanatakiwa kujitokeza na kundi lao na kuonyesha vipaji siku hiyo na kama wakiibuka washindi wa siku wataendelea na hatua zinazofuata.

Tags: