Ijumaa , 27th Mei , 2016

Msanii mkongwe wa Bongo fleva ambaye kwa sasa ameamua kujiingiza katika muziki wa Injili Stara Thomas amewataka wasanii na mashabiki kumuenzi rapa Albert Mangwea.

Msanii wa Bongo fleva na muziki wa Injili Stara Thomas

Akizungumzan na eNewz Stara alisema kuwa katika kipindi hiki kuelekea katika kukumbu ya kifo cha rapa huyo tumuenzi kwa yale mema aliyoyafanya huku akiwalaumu vijana wengi na wasanii kuona suala la madawa ya kulevya kama fasheni.

Pia Stara amesema kuwa kwa sasa yupo njiani kuachia wimbo wake wa dini na wa Bongo fleva pia kwa kuwa yeye anafanya miziki yote miwili kwa wakati mmoja hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kusubiri ngoma hizo ambazo moja ni ya kiroho na nyingine ni ya kidunia.