Ijumaa , 10th Mar , 2017

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kumshikilia msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee a.k.a Vee Money kwa tuhuma za kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya.

Vanessa Mdee

Kamanda wa Jeshi hilo, Kamishna Simon Sirro amesema kwa taarifa walizonazo, msanii huyo pamoja na watuhumiwa wengine, wanahusika na matumizi pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Sirro amesema msanii alikamatwa juzi jijini Dar es salaam, na upelelezi unaendelea.

"Tunamshikilia msanii Vanessa Mdee tangu Jumatano ambaye taarifa zinaonyesha kuwa ni mtumiaji lakini pia ni msambazaji wa dawa za kulevya, tunaendelea na uchunguzi wetu na tukikamilisha uchunguzi wetu na ikathibitika kama ana kosa la kujibu basi, tutamfikisha mahakamani". Amesema Sirro

Msikilize hapa Kamanda Sirro.