
Msanii Young Dee
Young Dee amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt cha EATV na kudai kitendo kilichotokea hakikuwa katika mipango yake hivyo sasa hivi kila mmoja ana maisha yake.
“Am single and am busy', sina mahusiano, ni kitu ambacho naweza kusema kibinadamu kinatokea kama baraka tu kwa sababu hakuwahi kuwa mpenzi wangu na imebaki kama ilivyokuwa mwanzoni” alisema Young Dee.
Katika upande mwingine, Young Dee amedai yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya ambao anaamini utakuwa mkali zaidi ya 'Bongo bahati mbaya' huku akisistiza kuwa ataendelea kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki bongo Mr T- Touch
Mtazame hapa Young Dee anavyofunguka zaidi..