Ijumaa , 1st Jul , 2022

Msanii Shilole amefunguka kuhusu rafiki yake wa muda mrefu Babalevo kwamba zamani baadhi ya watu walikuwa wanamkataa kwa sababua alikuwa anaomba omba sana. 

Picha ya pamoja ya Babalevo na Shilole

Akielezea ukaribu wake na Babalevo kupitia DADAZ ya East Africa TV Shilole amesema 

"Maji yakinifika hapa huwa namchana ukweli Babalevo ila ni sisi washkaji sana, unaweza kutuona mitandaoni tunachambana lakini baadaye ananiomba Elfu 20".

"Zamani watu walikuwa wanamkataa Baba Levo, walikuwa wanamuoa mtu wa ajabu anaombaomba sana, mimi nikasema huyu ni mtu wangu siwezi kumuacha sasa hivi huyu hapa amesimama".