
Picha ya msanii Shamsa Ford
Shamsa Ford amefunguka hilo kupitia WhatsApp status ambapo ameandika ujumbe ufuatao baada ya kupost picha ya rafiki yake Anita akiwa na mpenzi wake.
"Una bahati Anita, una mwanaume Billionaire, anakupa unachotaka , anakulea kama malkia, anakupenda na kukuheshimu aisee mshikilie, njoo Bongo tukuhadithie wanaume wetu ukiwaomba pesa wananuna"
"Yakiwa hayana eti yanasema nakupima, sasa unampima then shida zake ziende wapi, wahuni, waongo, hayana heshima.Wanaume wa kibongo msinitongoze sitaki, itabidi na mimi nivuke Tz nikatafute mwanaume kama wako" ameongeza
Shamsa Ford kwenye mahusiano yake ya nyuma aliwahi kuwa kwenye ndoa na Chidi Mapenzi pamoja na msanii Nay wa Mitego.