Jumanne , 1st Sep , 2015

Kufuatia kuanza rasmi kwa sheria mpya ya makosa ya mtandaoni Tanzania, wasanii wa muziki ambao wamekuwa kwa sehemu kubwa waathirika wa lugha za kashfa na kudhalilishwa katika mitandao, wametoa tathmini ya mapokezi ya sheria yenyewe.

staa wa muziki wa bongofleva Ney wa Mitego

Kwa kuangalia maoni mbalimbali ambayo wamekuwa wakipata kutoka kwa mashabiki wao katika siku hii ya kwanza.

Kama kipimo cha nguvu ya udhibiti wa makosa lugha za kashfa kwa njia ya mtandao, wasanii Ney wa Mitego, Ray C, kati ya wengine wameweka bayana kupungua na pia kwisha kabisa kwa lugha za kashfa na matusi ambazo wamekuwa wakitupiwa kama wanavyoeleza hapa.