Ijumaa , 14th Aug , 2015

Makundi 15 ya kudansi ambayo yamefanikiwa kupita katika hatua ya usaili wa mashindano ya Dance100% 2015 kwa mwaka 2015, leo hii yamefika katika ofisi za EATV kupigwa shule kuhusiana na taratibu zitakazotumika katika hatua inayofuata.

majaji wa shindano la Dance100% Shetta na Super Nyamwela wakitoa somo kwa washiriki 15 wa Dance100% 2015

Makundi hayo ni The Winners Crew, Mad Squad, The Heroes Crew, Mavuno Crew, Dream Team, Team ya Shamba, The WT Crew, W.D, Best Boys Kaka Zao, Team Makorokocho, Majokeri, Cute Babies, Wazawa Crew, Quality Boys na The Best, yamepata fursa adhimu kupata semina katika maandalizi yao kuelekea hatua ya robo fainali ya mashindano hayo makubwa ya kucheza Afrika Mashariki.