Ijumaa , 3rd Jul , 2020

Baada ya ku-trend kwa picha zake mitandaoni akiwa na mbunifu wa mavazi Martin Kadinda, Madam wa nchi na Staa wa filamu Wema Sepetu ametoa tahadhari kuhusu mguu yake na suala la kuvaa kigodogoro ili kuongeza ukubwa wa makalio yake.

Staa wa filamu hapa nchini Wema Sepetu

Kupitia picha hizo mashabiki na kurasa za kimbea walimjadili Wema Sepetu kwamba miguu yake ni mibaya na ameongeza kitu mwilini mwake kwani baadhi ya picha anaonekana hivyo na zingine haonekani akiwa hivyo.

"Tahadhari jamani natoa,  sipendi kusemwa miguu yangu maana mwenyewe najijua miguu mizuri, sikubarikiwa sababu hamnioni nikijishirikisha na vitu vya ushindani na mambo za huko chini, ndiyo maana wanasema Mungu hakupi vyote, wengine mnasema ukute miguu zenu ni vitu mbaya sana

Aidha akizungumzia kuhusu kuvaa kigodoro Wema Sepetu ameongeza kusema "Halafu hapo sijavaa kigodoro maana pia nimeona mnasema nimevaa ila waja hamna jema nyie"