'Young Dee umesahau Password'- Young Killer

Ijumaa , 8th Nov , 2019

Kupitia 'Insta story' ya mtandao wa Instagram, kumekuwa na ubishani wa kutambiana kati ya rapa Young Dee na Young Killer, kuhusu nani awe wa kwanza kuachia nyimbo zao mpya watakazozitoa hivi karibuni.

Kushoto pichani ni Young Dee na upande wa kulia ni Young Killer.

Ubishani huo ulikuwa unafanyika ndani ya studio za Touch Sound, chini ya Producer Mr T-Touch, ambapo Young Dee alinukuliwa akisema,

"Najaribu kumwambia Young Killer asitoe wimbo wake kesho kwa sababu na mimi natoa kesho, nishaweka maandalizi yangu au acha tuziachie tu sisi tumekaa miezi sita  bila kutoa ngoma" amesema Young Dee.

Ikumbukwe tu Young Dee, aliondoka nchini Tanzania na kwenda kuishi Marekani kwa muda wa miezi 6, bila kutoa ngoma huku akionekana akila bata pande hizo.
Aidha kwa upande wa Young Killer amemjibu Young Dee kwa kusema,

"Hapana wewe ndiyo usitoe kwa sababu umesahau namba za siri, mimi ndiyo natakiwa nitoe na tupo kwa wakala T-Touch, namba zangu za siri nazikumbuka wewe zako ushasahau acheni kwanza nitoe, nyie endeleeni kubana msiachie"  ameeleza Young Killer.

Hali hiyo ya kuwa pamoja ndani ya studio hizo za T-Touch, imeashiria kuwa sasa hivi hakuna tena bifu kati yao, kwani kipindi cha nyuma waliwahi kuwa na tofauti kuhusu ni nani mkali zaidi ya mwenzake.