Hakuna Simba bila Yanga - Gabo Zigamba

Jumatatu , 7th Nov , 2016

Msanii wa filamu nchini ambaye kwa sasa anatajwa kuwa ni moja kati ya waigizaji wanaofanya vizuri Gabo Zigamba amefunguka na kusema kuwa kati ya Simba na Yanga hakuna timu hata moja ambayo inam'boa' kwani timu hizo mbili zinategemeana sana.

Gabo akiwa Kikaangoni

 

Gabo Zigamba alisema hayo kupitia kipengele cha Kikaangoni ambacho huwa kinafanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, ambapo alidai kuwa bila uwepo wa Yanga haiwezi kuwepo Simba na bila uwepo wa Simba hakuwezi kuwa na Yanga. 

"Kati ya Simba na Yanga hakuna timu inayoni'boa', kwani hakuna Simba bila Yanga na wala hawezi kuwa Yanga bila Simba" alisema Gabo Zigamba 

Amesema kuwa hakuna timu anayoishabikia kati ya hizo