Jumatatu , 25th Apr , 2022

Raia wa Kenya, Yema Khalif na mkewe Hawi Awash wanatarajia kulipwa kiasi cha $150,000 sawa na Tsh million 348 katika mji wa California, Marekani baada ya kufanyiwa ubaguzi wa rangi na maofisa wa polisi katika mji huo.

Yema Khalif na mkewe Hawi Awash.

Mwaka 2020, Yema Khalif alifanyiwa ubaguzi wa rangi ndani ya duka lake katika mji wa California, polisi hawakuwa na imani kama yeye ndio mmiliki wa duka hilo, walitoa kauli za ubaguzi na kumuomba atoe funguo na nyaraka zinazoonesha kuwa yeye ndio mmiliki.

Mji wa California umekubali kulipa kiasi cha $150,000 kwa Yema Khalif na mkewe Hawi Awash kwa tukio hilo la mwaka 2020.