Jumapili , 22nd Dec , 2019

Waombolezaji  wa msiba katika kijiji cha Shambarere, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya wameshuhudia kisa cha maiti ambayo ilitakiwa ikazikwe, lakini ikashindikana baada viungo vyake vya mkononi kukunja ngumi kwa madai ya kutaka kulipwa mahari yake.

Jeneza

Baada ya mazungumzo baina ya pande zote mbili kutoka kwa mume aitwaye Malimu  na wazazi wa marehemu, zilidai maiti hiyo ilikuwa haijalipiwa pesa za mahari.

Kwa upande wa familia za mume huyo walikubali kulipa pesa ya mahari hiyo na baada ya hapo maiti ilikubali kukunjua mikono yake ambayo ilikuwa imekunja ngumi, kisha wazee kufanya maombi na mwili huo kuzikwa.

Source Citizen Tv.