Jumatano , 10th Jul , 2019

Katika mazingira ya kawaida hakuna binadamu ambaye hakosi wivu, kwa sababu uko kiasili na ni muhimu katika masuala mbalimbali.

Wapenzi

Lakini wivu ukizidi huwa na hasara zake, kwa leo tunaangazia wivu hasa katika mahusiano ya kimapenzi ambapo kupitia DADAZ ya EATV, Mtaalamu wa Saikolojia ya mwanadamu, Cosmas Madulu ameeleza faida na hasara za wivu katika mahusinao.

Kwanza bwana Cosmas anasema kuwa wivu unahitajika sana katika mahusiano, mmoja wapo katika mahusiano akiwa hana wivu kwa mwenzie basi ana tatizo la kisaikolojia lakini ukizidi pia ni hatari kwa wahusika,"wivu ni chakula cha nafsi ambacho kinamfanya mwanadamu kujihisi yuko salama. Faida ya kwanza inamfanya mtu kuwa salama, wanaume wana shida ya macho ya kupenda kila kitu kizuri wanachokiona kwahiyo anahitaji mwanamke ambaye anatmfanyia wivu ili amuweke salama", amesema Madulu.

Pia ameongeza kuwa faida ya pili ya wivu ni kuleta heshima katika mahusiano au ndoa. Kwenye faida za wivu katika mahusiano, bwana Madulu amesema, "wivu ukipitiliza unapelekea mauaji, mtu anaweza kutenda jambo ambalo halikutarajiwa kutokana na akili yake kufunikwa na hisia kubwa. Napenda mfahamu pia lugha 5 za mahusiano ambazo ni maneno matamu, kutumia muda pamoja", ameongeza.

Amemalizia kwa kuzitaja silaha kubwa mbili ambazo endapo mwanamke atazitumia, atadumisha mahusiano au ndoa yake, silaha hizo ni ngozi yake na masikio yake.

Tazama video zaidi hapa chini akizielezea.