Jumatatu , 9th Sep , 2019

Wanasayansi kutoka maabara ya Bristol Robotics, Uingereza mwaka 2017 waligundua njia mpya ambayo unaweza kuchaji simu kwa kutumia mkojo wako.

Simu ikichajishwa

Ili kuzalisha umeme walitengeneza kifaa maalum walichokipa jina la 'microbial fuel cell' ambacho kina bakteria wenye uwezo wa kuchuja chembechembe zote zinazopatikana katika mkojo na kubakiza elekroni maalum ambazo hubadilishwa kwaajili ya kuwa umeme kwaajili ya matumizi.

Lita mbili za mkojo zina uwezo wa kuzalisha nguvu ya umeme ya kiasi cha 30 mpaka 40 Milliwati ambayo inaweza kuiwasha simu, kuwasha taa na vifaa vingine vinavyotumia umeme.

Mpaka sasa uvumbuzi huo umezidi kufanyiwa utafiti kuhakikisha unaweza kuzalisha umeme mkubwa zaidi, huku malengo yake ni kwa nchi zinazoendelea ili kusaidia katika utunzaji wa mazingira na kupunguza ukosefu wa umeme unaozikabili nchi hizo.

Chanzo: BBC