Wanaume wawili wanaoishi na mwanamke mmoja

Jumatatu , 15th Jul , 2019

Habari ya wanaume wawili kutoka nchini Pakistan inaendelea kusambaa mitandaoni ikiwaonyesha wawili hao wakiwa katika uhusiano na mwanamke mmoja.

Wanaume wawili wanaoishi na mwanamke mmoja

Hii ni kutokana na picha iliyopandishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, na mtu aliejulikana kwa jina la Bazilk Khann na kuandika,

Mimi na rafiki yangu kipenzi tunampenda mwanamke mmoja, hatuwezi kupigana wala kugombana, ila tumekuja na makubaliano ya kuwa na mwanamke huyu mmoja na ndio urafiki wetu ulivyo.”

Katika picha hiyo inaonyesha wanaume hao wawili wakiwa 'super market' na mwanamke huyo, huku wote wakiwa wanam-busu pamoja.