Kushoto ni Kocha George Lwandamina , Kulia mchezaji Ajib akiwa anafanya mazoezi na timu yake mpya.
Licha ya Kocha huyo kutambua uwezo wa Ajibu amesema kwamba, mchezaji huyo anatakiwa kuonyesha kazi ya ziada mazoezini ili kuhakikisha hatasugua benchi kwa kujipatia namba.
"Mchezaji mpya anapoingia kwenye kikosi anakuwa ni plan mpya ya kocha, hivyo kuna jinsi ya ya kuwapa somo. Nafasi ya kucheza inaanzia na ushawishi kwa mchezaji mwenyewe. Mimi kocha ningependa wale watakaosaidia timu ndio nawapa kipaumbele . Kila anayefanya vizuri mazoezini, anakuwa na nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza," alisema Lwandamina.
Ajib amekuwa mshambuliaji mwenye kiwango cha hali ya juu akitokea Klabu ya Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Klabu ya wanajangwani



