Alando amebainisha hayo kwenye mkutano maalum wa waandishi wa habari uliofanyika muda mchache uliopita kwenye Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) ambapo Azam wanacheza mechi hiyo maalum ya kusherehesha ubingwa wa Ligi Kuu walioutwaa timu hiyo.
“Tunawashukuru sana wenzetu Rayon Sports kwa nafasi waliyotupa kucheza nao, wangeweza kuchagua timu nyingine lakini wametuchagua sisi ni jambo zuri, tunachoahidi ni soka safi kwa mashabiki. Najua wenzetu wamejipanga kuwa na furaha mara mbili, moja watakapokuwa wakikabidhiwa kombe na nyingine wakitaka kupata ushindi, lakini sisi tumejipanga kuwapa machungu kwa kuwafunga,” amesema Lea.
Pamoja na hayo, Alando amekitaja kikosi chake kitakachoshuka dimbani leo kuwa ni Mwadini Ally, Ismail Gambo, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, David Mwantika, Frank Domayo, Abdallah Masoud, Mudathir Yahya, Yahaya Mohammed, Yahya Zayd, Idd Kipagwile huku wachezaji wa akiba wakiwa Metacha Mnata, Benedict Haule, Abbas Kapombe, Joseph Kimwaga, Joseph Mahundi, Ramadhan Mohammed, Abdul Omary, Stanslaus Ladislaus, Godfrey Elias.
Mara baada ya mchezo huo, kikosi hicho kitaanza safari ya kurejea nchini siku ya Jumapili ili kuweza kuendelea na ratiba zake za mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.



