Alhamisi , 29th Oct , 2020

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Oktoba27,2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo.

Bernard Morrison ametozwa faini ya laki tano na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting FC

Ligi Kuu ya Vodacom Mechi namba 50: Tanzania Prisons FC 1-0 SimbaSC

Timu ya Tanzania Prisons FC imepigwa faini ya sh.500,000 (laki tano)kwa kosa la kuingiza uwanjani magari ya viongizi na mashabiki wakati mchezo ukiwa unaendelea

 

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45(1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

 

Mechi namba 50: Tanzania Prisons FC 1- 0 Simba FC, Mchezaji wa timu ya Tanzania Prisons Salum Kimenya ametozwa faini ya Sh.500,000 (laki tano)

na kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Simba BenardMorrison,katika mchezo uliochezwa Oktoba 22, 2020 kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.

 

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 39:2 (2.6) ya Ligi kuhusu udhibiti wa Wachezaji.

 

Mechi namba 50: Tanzania Prisons FC 1- 0 SimbaSC Mwamuzi Shomari Lawi amefungiwa miezi 12 kwa kushindwa kuumudu mchezo tajwa, aliochezesha Oktoba22,2020 katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.

 

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40 (4) ya Ligi Kuu kuhusu

udhibiti wa waamuzi.

Mechi namba 50: Dodoma Jiji FC 0-0 Mbeya City FC.

 

Klabu ya Dodoma Jiji imetozwa faini ya sh.500,000(laki tano) kwa kosa la kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo kupitia mlango wa nyuma ambao kimsingi si mlango rasmi wa kuingilia.

 

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 15 (54) ya Ligi

Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

 

Polisi Tanzania FC 1-1 Gwambina FC

 

Klabu ya Gwambina imetozwa faini ya sh.3,000,000(milioni tatu) kwako kucheza dakika zote tisini bila ya kuvaa nembo ya mdhamini.

 

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14 (1.6) ya Ligi Kuu kuhusu udhamini.

 

Mchezaji wa Polisi Tanzania FC, Daruwesh Saliboko ametozwa faini ya (laki tano) na kufungiwa michezo mitatu baada ya kutolewa mchezoni

kwa kadi nyekundu na mwamuzi kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa timu pinzani.

 

Mechi namba 34 :Simba SC 0-1 Ruvu Shooting FC

Mchezaji wa SimbaSC ,Bernard Morrison ametozwa faini ya sh.500,000 laki tano na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting FC JumaNyoso.

 

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 39 (5) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.

 

Mchezaji wa Ruvu Shooting FC, Juma Nyoso ametozwa faini ya sh.500,000 (laki tano) na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumkanyaga mguuni kwa makusudi mchezaji wa Simba SC Bernard Morrison mchezo ukiwa umesimama.

 

Mchezaji wa Ruvu Shooting FC Shabani Msala ametozwa faini ya (lakitano) na kufungiwa mechi tatu kwakosa la kumpiga teke mchezaji wa SimbaSC, Bernard Morrison.

 

Mechi namba 70 :KMC FC 1-2 Young Africans SC.

Mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani Kayoko amekumbushwa kuongeza

umakini katika majukumu yake ya kusimamia sheria za

mpira wa miguu.

Ukumbusho huo uliofanyika baada ya mchezo uliochezwa Oktoba25,2020

katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, umetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.