Jumanne , 7th Dec , 2021

Mchezaji wa tennis Novak Djokovic amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Serbia kwa ajili ya michuano ya ATP Cup inayotarajiwa kuanza mwezi January, 2021 mjini Sydney nchini Australia huku suala la kutochanjwa likibaki kuwa kitendawili.

(Nyota wa Serbia, Novak Djokovic))

Kujumuishwa kwa Djokovic 34, kumeleta sintofahamu baada ya kushindwa kuthibitisha kushiriki kwenye michuano ya Australia Open kutokana na kuwepo kwa sheria inayowalazimiu washiriki kupata chanjo ya Covid-19 na ambao wasiochanja kutoshiriki

Jambo hilo limepelekea baba mzazi wa Novak Djokovic wiki iliyopita kuthibitisha mwanae kutotetea ubingwa wake wa michuano hiyo ikiwa na tafsiri kuwa bado hajachanja.

Mbali na sakata hilo, taarifa za kikachero zinaripoti kuwa, huenda Djokovic ataombewa kibali maalumu sambamba na kujitenga kwa siku 14.

Serbia wamepangwa kundi A sambamba na Norway, Chile na  Spain huku michuano hiyo ikishirikisha  timu 16 huku viwanja viwili vikitumika kwenye michezo hiyo inayotarajiwa kuanza junuary 1 mpaka 9 mwaka 2022.