Jumapili , 6th Aug , 2017

Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Felix Simbu ameshinda medali ya shaba baada ya kushika nafasi ya tatu katika mbio ndefu za marathoni kwenye mashindano ya dunia yanayoendelea kufanyika Jijini London Nchini Uingereza kwa siku ya tatu leo.

Bendera ya Tanzania.

Geofrey Kirui anayetokea nchi ya Kenya ameshika nafasi ya kwanza na kupata medali ya dhahabu huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mwanariadha kutoka nchi ya Ethiopia Tamirat Tola na kupata medali ya fedha.

 Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Felix Simbu.

Kwa upande mwingine nchi ya Tanzania imewakilishwa na Alphonce Felix Simbu, Ezekiel Jafary na Stephano Gwandu Huche kwa upande wa wanaume huku wanawake wakiwa ni Sara Ramadhani pamoja na Magdalena Shauri kwa wanawake.

 Kwa ushindi huo, Simbu anakuwa anaiandikia historia nchi ya Tanzania ya kuwa Mtanzania wa kwanza tangu mwaka 2005 kunyakua medali ya shaba kwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya riadha ya dunia yanayofanyika nchini Uingereza.