Jumatano , 2nd Nov , 2016

Kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona jana usiku kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema hawakucheza na Barcelona bali wamecheza na timu ya utamaduni wao.

Pep Guardiola

 

Mabao mawili ya Ilkay Gundogan na Kevin De Bruyne, yalitosha kuifikisha City kwenye nafasi ya pili, ikiwa na pointi 7, nyuma ya Barcelona yenye pointi 9, na hivyo kujiwekea mazingira ya kutinga 16 bora endapo itashinda mechi mbili zilizobaki.

Kwengineko Mesut Ozil alifunga bao la dakika za mwisho na kuwawezesha Arsenal kutoka nyuma 2-0 na kulaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa mabao 3-2 na kuwafikisha hatua ya mtoano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Ozil alionekana kutulia alipokimbia langoni, akampiga chenga kipa na mabeki wawili na kisha akatumbukiza mpira kimiani.