
Wachezaji wa Manchester City wakishangilia moja ya bao awlilofunga usiku wa jana dhidi ya Borussia Monchegladbach.
Manchester City imefuzu hatua hiyo kwa mabao ya jumla 4-0 baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua iliyopita ya 16 bora kupata ushindi wa mabao 2-0 .
Mabao ya City yamefungwa na nahodha wake Kelvin De bruyne dakika ya 11 kwa shuti kali na dakika 6 baadae kiungo Ilkay Gundogan alifunga bao la pili na kuihakikishia Manchester City kufuzu hatua hiyo.
Pep amesema “Wakati mwingine inaonekana ni rahisi sasa baada ya mchezo kumalizika. Kilikuwa ni kiwango kizuri, tulikuwa na umiliki wa mchezo kwa dakika zote 90 na tuliwasili hapa tukiwa na matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza, lakini michuano hii ina mtego”.
“Tupo makini sana” Pep akamalizia.
Kwa upande wa kocha wa Borussia Monchengladbach, Marco Rose amesema “Tulikuwa na hali ya kujiamini sana lakini tunapaswa kutambua kuwa mpinzani alikuwa imara sana kwetu”.
“Timu ilijitahidi kufanya kadri iwezavyo. Tulipata nafasi ya kufanya majaribio yaliyolenmga lango lakini kama ukiiruhusu City kufanya majaribio zaidi huwezi kufika mbali. Tulipaswa kutumi anafasi tulizotengeneza”.
“Kitu muhimu kwangu licha ya Manchester City walituzidi uwezo sana, ni namna wachezaji walivyoweka juhudi kwenye mchezo na kusimama imara licha ni ngumu kucheza dhidi yao”.
Kipigo hiko kimeifanya Borussia Monchengladbach kupoteza mchezo wake wa saba mfululizo kwenye michuano yote ikiwa ni kiwango kibovu kuwahi kutokea kwenye historia ya klabu hiyo.
Manchester City imeungana na Real Madrid ya Hispania, Borussia Dortmund ya Ujerumani, FC Porto ya Ureno, PSG ya Ufaransa na Liverpool ya England kutinga hatua ya robo fainali.
Droo ya nani kucheza na nani kwenye hatua ya robo fainali pamoja na ile ya nusu fainali inatazamiwa kupangwa siku ya Ijumaa ya tarehe 19 Machi 2021 nchni Uswizi.