Jumapili , 15th Nov , 2020

Lewis Hamilton ameshinda ubingwa wa dunia wa mbio za magari 'Formula1' mwaka 2020, baada ya kuongoza mbio za Uturuki (Turkish Grand Prix), zilizomalizika mchana wa leo Novemba 15, 2020.

Lewis Hamilton

Hamilton ambaye ni derewa wa timu ya magari ya Mercedes, sasa amechukua ubingwa huo kwa mara ya 7 na kuifikia rekodi ya nguli Michael Schumacher.

Raia huyo wa Uingereza mwenye miaka 34, ameshinda ubingwa zikiwa zimebaki mbio mbili kukamilisha msimu wa 2020. Mbio zilizobaki ni za Bahrain (Sakhir Grand Prix) ambazo zitafanyika Desemba 4 huku zile za mwisho zikiwa ni Yas Marina, Abu Dhabi (Abu Dhabi Grand Prix) ambazo zitafanyika Ijumaa Desemba 11.

Madereva mbalim,bali wakimpongeza Lewis Hamilton

Katika mbio za leo za Uturuki, Lewis ameongoza huku dereva mwenzake kutoka timu ya Mercedes Valtteri Bottas.

Lewis Hamilton - Mercedes
Sergio Perez - Racing Point
Sebastian Vettel - Ferrari
Charles Leclerc - Ferrari
Carlos Sainz - McLaren
Max Verstappen - Red Bull
Thailand Alexander - Red Bull    
Lando Norris - McLaren
Lance Stroll - Racing Point
Daniel Ricciardo - Renault

Kushoto ni Michael Schumacher na kulia ni Lewis Hamilton

Lewis Hamilton amechukua ubingwa huo mwaka 2008, 2014, 2015, 2017, 2018, 2019 na 2020.
Schumacher yeye amechukua ubingwa mwaka 1994, 1995, 2000, 2001, 2002, 2003 na 2004