Jumamosi , 8th Dec , 2018

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amethibitisha kurejea kikosini kwa mlinzi mkongwe wa timu hiyo Kelvin Yondani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Kushoto ni Kelvin Yondani na kulia ni Ibrahim Ajibu

Akiongea leo kuelekea mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Biashara United kesho, kwenye uwanja wa taifa, Zahera amesema wachezaji watatu wamepona akiwemo Yondani.

"Wachezaji watatu wamerejea kwenye kikosi na wamefanya mazoezi na timu hivyo watakuwa sehemu ya mchezo wa kesho. Wachezaji hao ni Papy Tshishimbi, Gadiel Michael na Kelvin Yondani." amesema Zahera.

Licha ya kurejea kwa nyota hao Zahera pia amesema mshambuliaji Ibrahim Ajibu hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho pamoja winga Mrisho Ngassa ambao wanatumikia adhabu za kadi.

Heritier Makambo ana asilimia 50 ya kuweza kushiriki mchezo wa kesho baada ya kupata maumivu kwenye mazoezi ya leo asubuhi, lakini Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngasa wao moja kwa moja hawatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho ila  "

Kuhusiana na wapinzani wao,  Zahera amesema wamejindaa vizuri wakitambua kuwa kila mara timu kubwa inapocheza na timu ndogo ambazo zipo chini kwenye msimamo huwa kuna hali ya kukamiwa sana.