Jumatano , 9th Dec , 2020

Klabu ya Manchester United ya Uingereza imeondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya klabu ya RB Leipzig kwenye mchezo wa mwisho kukamilisha hatua ya makundi ya michuano hiyo usiku wa hapo jana.

Mashabiki wa Manchester United wakionekana kusikitika baada ya kupoteza mchezo (zamani) .

Man Utd walihitaji alama 1 tu ili kufuzu kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora ya michuano hiyo lakini walikutana na upinzani mkali mbele ya vijana wa kocha Julian Nagelsmann na kuanza kuandika bao la kwanza mapema dakika pili ya mchezo kupitia mlinzi wao wa kushoto Angelino.

RB Leipzig wakapata bao la pili kupitia Mlinzi wake wa kulia Haidara dakika ya 11 na kabla ya Willi Orban kufunga bao na kukataliwa. Justin Kluivert aliwafungia Leipzig bao la tatu dakika ya 69 na kuwaongezea uongozi na kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua inayofuata.

Man Utd walifanikiwa kupata mabao 2 kupitia kwa Bruno Fernandes kwa mkwaju wa penalti na Paul Pogba na kubadilisha mchezo baada ya kufanya mabadiliko ya kuwaingiza Paul Pogba, Donny Van de beek, Paul , Axel Tuanzebe, Brandon Williams na Timothy Fosu Mensah.

Baada ya matokeo hayo msimamo wa kundi H ukachukua taswira nyingine, RB Leipzig akienda kileleni akiwa na alama 12, PSG akishika wapili kwa alama 9 na wawili wakifuzu ilhali Man Utd akishika nafasi ya tatu na kudondokea Europa league na kumuacha Istanbul Basaksehir kushika mkia.

Kwanini PSG Wamefuzu ilhali wana alama 9 sawa na Man Utd?

Man Utd licha ya kuwa alama 9 sawa na wapili PSG ambaye amefuzu, Utd haijafuzu kwasababu ya sheria inayoangalia utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa kwenye michezo miwili ambayo wanaofanana alama wamecheza. (Head to Head Goal Difference)

Kwa mujibu wa sheria hiyo, PSG amefikishika mabao 4 na Man Utd mabao 3 baada ya Man Utd kushika 2-1 Mchezo wa kwanza dhidi ya PSG na PSG kuifunga Man Utd mabao 3-1 kwenye mchezo wa pili wa marudiano wa michuano hiyo.

Ubaguzi waendelea kushika kasi michezoni Ulaya

Klabu ya Istanbul Basaksehir ya nchini Uturuki imeripoti kisa kimoja cha ubaguzi wa rangi wakiwa uwanjani kuendelea na mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya klabu ya PSG ya Ufaransa ambao haukumalizika.

Wakati mchezo unaenedelea dakika ya 14 kocha msaidizi wa Istanbul Pierre Webo alioneshwa kadi nyekundu na kutakiwa kutoka uwanjani baada ya kuonekana kutupiana Maneno ya mwmuzi wa akiba Sebastian Coltescu wa Romania.

Mshambuliaji aliyekuwa benchi wa klabu hiyo Demba Ba amenukuliwa akimhoji mwamuzi hiyo wa akiba akiswma “Kwanini useme ni mtu mweusi” jambo lililopelekea wachezaji wa Istanbul Kuchukizwa na kutoka uwanjani dakika ya 23 na wachezaji wa PSG na wao kutoka uwanjani.

Mchezo huo unarudia hii leo kwa dk76 zilizosalia licha ya PSG kufuzu kufuatia Man Utd kufungwa.